Skip to main content

Posts

Showing posts with the label OLAS

Search

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA AWAMU YA NNE, UHAMISHO NA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA ASTASHAHADA (CHETI) NA STASHAHADA (DIPLOMA) KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA AWAMU YA NNE, UHAMISHO NA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA ASTASHAHADA (CHETI) NA STASHAHADA (DIPLOMA) KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017 Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu Waombaji wote walioomba kudahiliwa katika kozi za Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma) na Umma kwa ujumla kuwa dirisha la maombi lilifungwa mnamo tarehe 15 Oktoba 2016 ili kuruhusu uteuzi wa awamu ya nne kwa waombaji wa kozi hizo. Uteuzi wa awamu ya nne kwa waombaji wa Astashahada na Stashahada unatarajiwa kutangazwa mnamo tarehe 2 Novemba 2016 , hivyo basi waombaji wanaombwa kuwa na subira ili kutoa muda kwa Baraza kukamilisha taratibu za uteuzi huo. Maombi mapya ya Udahili: Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) utafunguliwa tena tarehe 2 Novemba 2016 hadi tarehe 6 Novemba 2016 ilikujaza nafasi za udahili zilizobaki wazi baada ya uchaguzi wa awamu ya nne. Hatua hii itaweze...